• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Hispania yaizamisha Canada na kuondoka na taji la Davis Cup

    (GMT+08:00) 2019-11-25 08:42:36

    Rafael Nadal ameifanya Hispania iondoke na ushindi wa kombe la Davis dhidi ya Canada baada ya kumzamisha Denis Shapovalov mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani mjini Madrid. Ushindi wake wa 6-3 7-6 (9-7) ulimfanya anyakue taji hilo, huku Mhispania Roberto Bautista Agut naye akirejea kwenye timu siku tatu baada ya kufiwa na baba yake na kuchochea ushindi huo wa Hispania. Bautista Agut alitiririkwa na machozi baada ya kumshinda Felix Auger-Aliassime mwenye miaka 19 kwa 7-6 (7-3) 6-3 katika mechi ya ufunguzi. Ushindi wa Nadal ukaifanya Hispania iwe mbele kwa 2-0 na kubeba taji la sita la Davis Cup. Michuano hiyo iliyojumuisha timu 18 na kufanyika kwa wiki nzima imeshuhudia mchezaji namba moja duniani akiisaidia Hispania kupata taji la kwanza tangu mwaka 2011 na kuwahakikishia mashabiki wenyeji wanaondoka kifua mbele kwa vifijo na nderemo kwenye Makala ya michuano hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako