• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Manchester United na Sheffield United hakuna mbabe baada ya kuondoka na sare ya mabao 3-3

  (GMT+08:00) 2019-11-25 08:43:03

  Manchester United na Sheffield United wametoshana nguvu baada ya kuondoka na sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliogaragazwa jana usiku Uwanja wa Bramall Lane. Sheffield United walitangulia kwa mabao ya John Fleck dakika ya 19 na Lys Mousset dakika ya 52, kabla ya timu ya Man Unitedwaliopo chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kucheza kwa dakika 70 huku wakiburutwa kwa mabao mawili ya wapinzao na ndani ya dakika 10 wakaamua kufanya maangamizi kwa kuanza na goli la kusawazisha la Brandon Williams dakika ya 72 na Mason Greenwood dakika ya 77 na hatimaye Marcus Rashford kufunga la tatu dakika ya 79. Naye Oli McBurnie alifunga hesabu za siku baada ya kuifungia Sheffield United bao la kusawazisha dakika ya 90.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako