• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waokoaji wa Italia wagundua miili mitano ya wahamiaji haramu

  (GMT+08:00) 2019-11-25 09:32:02

  Polisi wa Pwani wa Italia wamesema kwamba waokoaji wamegundua miili mitano kwenye eneo la ajali ya meli ya wahamiaji haramu kusini mwa Italia na pwani ya karibu.

  Meli iliyobeba wahamiaji haramu ilipinduka na waokoaji wa Italia wameokoa watu 149, wakiwemo wanawake 13 na watoto watatu. Waliookolewa wamesema bado watu wapatao 20 ambao hawajulikani walipo.

  Taarifa iliyotolewa na Walinzi wa Pwani nchini Italia imesema miili yote ni ya wanawake na hadi sasa kazi ya utafutaji na uokoaji bado inaendelea, lakini hali mbaya ya hewa imesababisha kazi hiyo kuwa ngumu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako