• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Japan zakubaliana kukuza uhusiano na kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo

    (GMT+08:00) 2019-11-25 16:59:12

    Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi wamekutana leo mjini Tokyo na kukubaliana kuwa nchi hizo zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kukuza uhusiano wao na kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo.

    Bw. Abe amesema Japan inatumai kuwa ziara ya rais Xi Jinping wa China itakayofanyika nchini humo mwakani itakuwa ni fursa mpya kwa kuhimiza uhusiano wa nchi hizo mbili katika zama mpya. Amesema uhusiano tulivu kati ya Japan na China ni msingi wa amani na ustawi barani Asia, na pia ni muhimu katika kushughulikia changamoto za sasa za dunia, hivyo Japan iko tayari kufanya kazi na China kupanga mustakabali mzuri mpya kwa nchi hizo mbili.

    Kwa upande wake, Bw. Wang amesema kutokana na maelekezo ya kisiasa ya viongozi wa nchi hizo mbili na juhudi za pamoja, uhusiano kati ya China na Japan umerudi kwenye njia sahihi na kupata maendeleo. Ametoa wito kwa Japan kufanya kazi kwa pamoja na China, kuchukua hatua chanya, na kushughulikia vizuri tofauti za nchi hizo ili kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya ajenda kuu za kisiasa na kidiplomasia zilizoandaliwa za nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako