• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Bure kushuhudia pambano la Mwakinyo na Mfilipino Dar

  (GMT+08:00) 2019-11-25 18:18:13

  Mabondia Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay wamekutana kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki katika viwanja vya Leaders Club, siku nne kabla ya pambano lao, na kutangaza pambano hilo kuwa bure kabisa pasipo kiingilio chochote. Mwakinyo atapambana na mpinzani wake Novemba 29 katika pambano la raundi 10 la uzani wa welter litakalofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Hassan Mwakinyo amesema kuwa aliomba pambano hilo lisiwe na kiingilio ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kujitokeza kumshuhudia siku hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako