• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Harambee Starlets wateuliwa kuwania tuzo la CAF baada ya kuponda Burundi 5-0

  (GMT+08:00) 2019-11-25 18:19:36

  Vipusa wa timu ya soka ya taifa ya Kenya kwa upande wa Wanawake Harambee Starlets wameteuliwa kuwania tuzo ya timu bora ya wanawake mwaka huu, muda mfupi baada ya kupata matokeo bora dhidi ya Burundi. Starlets wamejikatia tiketi kwenye mashindano ya soka ya wanawake ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kwa ushindi wa mabao 5-0 waliopata dhidi ya Burundi Jumamosi iliyopita. Warembo hao wa Kenya walitumia muda wa dakika 14 pekee kufungua ukurasa wa mabao kupitia kona iliyochongwa na nahodha Dorcas Shikobe na kisha kufululiza kwa kichwa hadi kimyani hivyo kuweka Kenya kifua mbele. Ushahuri wa David Ouma kwa kikosi chake muda wa mapumziko uliwachochea Starlets kuwalipua Burundi kipindi cha pili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako