• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Exim Bank Tanzania yafungua tawi Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-11-25 18:45:37

    Benki ya Exim Tanzania imezidi kujitanua zaidi nje ya mipaka ya Tanzania kwa kufungua kituo cha huduma za benki hiyo (Commercial Representative Office) katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.

    Kauli hiyo imetolewa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk Bernard Kibesse wakati akifungua rasmi tawi jipya la benki ya Exim Tanzania lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam ikiwa ni baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.

    Kufuatia hatua hiyo, Benki hiyo inakuwa taasisi ya kwanza ya kifedha nchini Tanzania kuendesha shughuli zake kwenye mtandao wa mataifa matano ikiwemo Ethiopia ambayo inatajwa kuwa ndio nchi ya pili kwa ukubwa wa idadi ya watu barani Afrika.

    Mataifa mengine ambayo benki hiyo inaendesha huduma zake ni pamoja Uganda, Comoro na Djibouti.

    Taarifa ya benki hiyo imesema tayari imepata leseni ya kufungua na kuwa na Ofisi ya Mwakilishi wake nchini Ethiopia kupitia tawi lake la nchini Djibouti na imepanga kuanza kazi kutoa huduma zake nchini humo hivi karibuni.

    Amesema upanuzi huo wa Ethiopia unakuja kama sehemu ya mikakati wa upanuzi wa benki hiyo kwa ujumla katika kutimiza matarajio yake ya kuwa Benki ya Pan African.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako