• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yafichuka jinsi watumishi wa umma wanavyofyonza nchi

  (GMT+08:00) 2019-11-25 18:46:21

  Watumishi wa umma wanaendelea kufyonza nchi kupitia marupurupu wanayodai kila mwezi kwa kazi waliyoajiriwa kutekeleza yanayowafanya wapate mishahara minono bila kuchoka.

  Hii inafanya mfanyakazi wa serikali ya Kenya kupata mshahara wa wastani wa Sh78,000 kila mwezi na kuwa wanaopata mshahara bora zaidi katika nchi za eneo hili.

  Kulingana na Tume ya Mishahara na Marupurupu nchini (SRC), Kenya hutumia Sh795 bilioni kila mwaka kulipa wafanyakazi wa umma wapatao 842,900 mishahara yao.

  Hii inamaanisha kuwa, kwa wastani, wafanyakazi wote wa umma wangelipwa mishahara sawa, kila mmoja angepata Sh930,000 kwa mwaka.

  Mwenyekiti wa SRC, Lyn Mengich, anasema kwamba japo Wakenya hudhani mishahara ya watumishi wa umma ni ya chini, kuna wanapata mishahara minono kila mwezi kwa sababu ya marupurupu. Ingawa watumishi wa umma huwa wanadai marupurupu kwa kazi waliyoajiriwa kufanya, hakuna anayewachukulia hatua.

  Utafiti wa SRC ulifichua kuwa kuna aina 149 za marupurupu wanayolipwa watumishi wa umma ambayo wanatumia ujanja kufyonza walipa ushuru.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako