• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu

    (GMT+08:00) 2019-11-25 19:42:19

    China imetoa waraka wa "mapendekezo ya kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu" ili kupanga kazi ya kulinda haki hizo katika zama mpya. Mamlaka ya ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu ya China imesema, China inaheshimu na kulinda hakimiliki za kiubunifu za nchi za nje, pia inataka nchi za nje zilinde haki hizo za China.

    China imeshiriki kwenye karibu makubaliano yote ya kimataifa kuhusu hakimiliki za kiubunifu, kusaini makubaliano na kumbukumu na nchi na mashirika zaidi ya 60 duniani, na kuanzisha rasmi ushirikiano na nchi wanachama 50 wa Shirika la Kimataifa la Hakimiliki za Kiubunifu.

    Kwa mujibu wa "mapendekezo ya kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu" yaliyotolewa hivi karibuni, China itaongeza zaidi ushirikiano wa kimataifa, kukamilisha njia ya mawasiliano na wamiliki wa haki hizo kuimarisha huduma za msaada nje ya China, kuboresha na kuratibu mfumo wa kupasha habari. Naibu mkurugenzi wa mamlaka ya hakimiliki za kiubunifu ya China Bw. Gan Shaoning anasema,

    "Tunaheshimu na kulinda hakimiliki za kiubunifu za nchi za nje, pia tunatumai kuwa serikali za nchi za nje zinalinda hakimiliki za kiubunifu za China. Tutakamilisha, hatua kwa hatua, utaratibu wa kuwasiliana na makampuni binafsi ya China haswa yale madogo na yenye ukubwa wa kati, na makampuni ya nchi za nje yaliyo nchini China. Tutayatendea makampuni yote kwa usawa, na kuanzisha mazingira mazuri ya kiuvumbuzi na kibiashara."

    Hadi sasa China imejenga mfumo wa sheria za kulinda vizuri hakimiliki za kiubunifu, na kuzingatia ulinzi kwa hakimiliki hizo katika sekta maalumu za nchi zilizoendelea na zinazoendelea, hatua iliyopongezwa sana na jumuiya ya kimataifa. Ripoti ya Mwaka 2020 ya Mazingira ya Kibiashara Duniani iliyotolewa na Benki ya Dunia inasema China inashika nafasi ya 31 duniani kwa ubora ya mazingira ya kibiashara.

    Waraka mpya uliotolewa na China pia umezingatia ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu za China katika nchi za nje. Bw. Gan anasema,

    "Tutajenga jukwaa husika ili kuimarisha nguvu ya kulinda hakimiliki zetu za kiubunifu katika nchi za nje. Pia tutaongeza uratibu na kukamilisha huduma, na kujenga kituo cha maelekezo ya kukabiliana na mivutano ya hakimiliki za kiubunifu nje ya China, ili kulinda maslahi ya makampuni ya China yaliyoko nchi za nje."

    Waraka huo pia umeagiza kuboresha na kukamilisha mfumo wa ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu, kuimarisha ulinzi huo kwa njia ya kisheria, kisiasa, kiuchumi, kiteknoloja na kijamii, ili kuinua kiwango cha ulinzi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako