• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na ujumbe wa Chama cha United cha Russia

  (GMT+08:00) 2019-11-25 20:55:24

  Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na ujumbe wa Chama cha United cha Russia katika Ukumbi wa Mikutano wa Umma mjini Beijing.

  Ujumbe huo unaoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Juu la Chama cha United Bw. Boris Gryzlov, uko Beijing kuhudhuria mkutano wa 7 wa mfumo wa majadiliano kati ya vyama tawala vya China na Russia.

  Katika mazungumzo yao, rais Xi amesema yeye na rais Vladmir Putin wa Russia wametangaza kwa pamoja kuanzishwa kwa uhusiano wa kina wa kimkakati wa uratibu katika zama mpya kati ya China na Russia, pia walikubaliana kuongoza uhusiano wa pande mbili katika mwelekeo wa kuungana mkono, maingiliano ya kina, na ushirikiano wa uvumbuzi ili kutimiza matokeo ya kunufaishana kwa pande zote. Amesema nchi hizo mbili zimeunda ushirikiano thabiti wa kuungana mkono, ambao una umuhimu mkubwa kwa ajli ya amani na maendeleo ya dunia.

  Kwa upande wake, Gryzlov amesema uhusiano wa nchi hizo mbili umefikia ngazi isiyotarajiwa kwa kuwa nchi hizo zina ushirikiano thabiti katika nyanja mbalimbali na uratibu mzuri katika masuala muhimu ya kimataifa na kikanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako