• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka unaoweka wazi ukosefu wa usawa wa kijinsia nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2019-11-26 16:59:12

    Kituo cha Elimu ya Haki za Binadamu cha China kimetoa waraka uliopewa jina la "Suala la ukosefu wa usawa wa jinsia nchini Marekani ni kikwazo kikubwa cha kutimiza haki za wanawake nchini humo" hii leo. Waraka huo umesema, Marekani bado haijafanyia marekebisho Mkataba wa Kuondoa Aina Zote za Kutengwa kwa Wanawake, ambao ni moja ya mikataba mikuu ya haki za binadamu nchini humo, na wala haijasuluihisha tatizo kubwa la nchi hiyo la ukosefu wa usawa wa kijinsia, na kuongeza kuwa, jambo hili limezuia kwa kiasi kikubwa kutimia kwa haki za wanawake nchini Marekani.

    Waraka huo umeainisha kuwa, ukosefu wa usawa wa kijinsia ni tatizo kubwa sana katika jamii ya Marekani, na wanawake nchini humo wameteseka kwa muda mrefu kutokana na kutengwa kimfumo, kwa upana wake, kijamii na hata kwa siri, hususan katika ukosefu wa usawa wa kijinsia kiuchumi, uhalifu mkubwa dhidi ya wanawake, na ukosefu wa ulinzi kwa haki ya afya kwa wanawake walioko kwenye makundi madogo.

    Marekani ni nchi iliyoendelea zaidi kiuchumi duniani, lakini imeshindwa kulinda haki za wanawake kiuchumi ndani ya nchi hiyo, na kutokana na hilo, wanawake nchini Marekani wanakabiliwa na kutengwa katika kupata ajira, mishahara, na kuendeleza ujuzi wao.

    Kuhusu uhalifu dhidi ya wanawake, waraka huo umesema mmoja kati ya wanawake watatu nchini Marekani ameathiriwa na ukatili wa majumbani. Wanawake walioko jela wanateseka na ukatili mkubwa. Askari wanawake mara nyingi wanakuwa ni wahanga wa unyanyasaji wa kingonoi wakati wakiwa kazini. Ukinukuu hojaji mbalimbali, waraka huo umesema zaidi ya asilimia 32 ya wanawake katika jeshi la Marekani wamesema wamenyanyaswa kijinsia, na asilimia 80 wamesema wamesumbuliwa kijinsia.

    Tatizo kubwa la ukosefu wa usawa wa kijinsia nchini Marekani linatokana na sababu mbalimbali, ikiwemo historia ya utamaduni wa kuwatenga wanawake, mfumo dume, na haswa, mapungufu katika mfumo kijamii nchini humo, ambao unasababisha vizuizi vya kuondoa tatizo hilo. Pia waraka huo umeonyesha kuwa, kwa miaka kadhaa, Marekani imekuwa ikitekeleza vigezo viwili kuhusu suala la haki za binadamu, ikitumia haki za binadamu kama kifaa cha kudumisha umwamba duniani, kukosoa nchi nyingine, na kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, wakati ikipuuza tatizo lake lenyewe kubwa kuhusu haki za binadamu.

    Waraka huo umesema, kile ambacho Marekani imefanya kinakinzana na thamani na malengo yanayohusiana na haki za binadamu, na kuongeza kuwa Marekani imeendelea kuwa msumbufu na mvurugaji wa haki za binadamu katika nyanja ya kimataifa, na imevuruga sana maendeleo ya utulivu ya haki za binadamu kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako