• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwandamizi wa China alaani Marekani kupitisha muswada kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-11-26 19:09:43

    Mkurugenzi wa ofisi ya kisiasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Yang Jiechi amefafanua msimamo imara wa China wa kupinga vikali bunge la Marekani kupitisha muswada wa "haki ya binadamu na demokrasia ya Hong Kong".

    Bw. Yang amesema, mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, nguvu yoyote ya nje hairuhusiwi kuingilia kati mambo hayo. Amesema China itaendelea kulinda uhuru, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, kutekeleza sera ya 'China Moja Mifumo Miwili' na kupinga uingiliaji wa nje katika mambo ya Hong Kong.

    Habari zinasema, polisi wa Hong Kong wametoa wito kwa watu waliokalia Chuo Kikuu cha Polytechnic cha Hong Kong (PolyU) kuondoka mapema kwa amani. Pia wanaendelea kuwasiliana na chuo hicho wakisisitiza kupenda kutatua suala hilo kwa njia rahisi na ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako