• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ataka kutungwa kwa makini mpango wa 14 wa miaka mitano kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii

    (GMT+08:00) 2019-11-26 19:47:29

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo ameitisha mkutano wa kupanga kazi ya kutunga mpango wa 14 wa miaka mitano kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii.

    Bw. Li amesema katika kipindi cha mpango wa 14 wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025, mazingira ya nje yatakabiliwa na sintofahamu na changamoto nyingi zaidi, na China itakuwa katika kipindi muhimu cha kubadilisha njia ya maendeleo, kuboresha muundo wa kiuchumi na kutafuta injini mpya za ukuaji.

    Amesisitiza kuwa maendeleo yanatakiwa kupewa kipaumbele kwenye mpango huo, kuweka msisitizo uchumi ukue kwa kasi inayofaa na kwa ubora zaidi, kuweka msisitizo kwenye maslahi ya watu, na kuwekea msisitizo nafasi muhimu ya mageuzi na uvumbuzi katika kutatua matatizo ya maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako