• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa madini wahamia Arusha

    (GMT+08:00) 2019-11-26 19:57:03

    Wafanyabiashra wa madini zaidi ya 1,000 wakiwamo wakubwa,wa kati,na wadogo,katika soko la madini jijini Arusha,wameitikia wito wa serikali wa kuhamia katika soko hilo.

    Licha ya kuitikia wito huo,wameiomba serikali kuboresha miundombinu,ikiwamo huduma ya vyoo ambayo hairidhishi na inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabishara wa Madini (TAMIDA),Sammy Mollel,alisema mwitikio wa wafanyabiashara umesababisha eneo la madini kufurika na kusababisha foleni ya magari.

    Mollel alisema tangu kuzinduliwa kwa soko hilo Juni mwaka huu,wafanyabiashara wameweza kupata faida kubwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa biashara ya madini kwenye masoko yote yaliyoanzishwa na serikali nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako