• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yatoa mafunzo ya kuhifadhi viazi Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-11-26 19:57:35

    Bodi ya Kilimo nchini Rwanda imesema inashirikiana na wataalamu wa kilimo kuleta teknolojia za bei nafuu ambazo zinaweza kusaidia kuhifadhi viazi kwa zaidi ya miezi sita.

    Bodi hiyo inasema imeanzisha mpango huo ili kuwa na utoshelevu wa chakula na pia kukabiliana na bei za chini zinazowaathiri wakulima.

    Rwanda huzalisha tani 916,000 za viazi kila mwaka,na kufanya zao hilo kuwa la tatu kwa uzalishaji nchini humo.

    Takwimu kutoka Taaisi ya Kitaifa ya Takwimu nchini Rwanda zinaonesha kuwa matumizi ya viazi kwa kila mtu ni kilo 125.

    Upande wa kaskazini unachangia zaidi ya asilimia 80 ya uzalishaji wa viazi nchini humo.

    Katika eneo hilo,viazi ndio chakula kikuu huku zaidi ya asilimia 60 ya uzalishaji viazi ikitumiwa kwa matumizi ya nyumbani.

    Hata hivyo,wakulima wa viazi mara kwa mara wanauza viazi vyao kwa bei ya kutupa wakati wa msimu wa mavuno kwa sababu hakuna mbinu za kuhifadhi viazi hivyo kwa muda mrefu ili kuuzwa baadae wakati bei ni nzuri.

    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kilimo Rwanda,Charles Bucagu,alisema uhamishaji wa mbinu za uhifadhi ndio suluhu ya changamoto hiyo.

    Aliyasema hayo jana wakati wa utoaji wav yeti kwa wakulima waliokuwa wamepewa mafunzo ya mbinu za kuhifadhi viazi,chini ya msaada wa serikali ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako