• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China asisitiza utekelezaji wa hatua muhimu za mkutano wa CPC

  (GMT+08:00) 2019-11-26 20:41:01

  Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Xi Jinping ameendesha mkutano wa 11 wa kamati kuu inayosimamia mageuzi ya kina uliofanyika leo.

  Xi, ambaye pia ni rais wa Jamhuri ya Watu wa China, amesisitiza utekelezaji wa hatua muhimu zilizofikiwa katika kikao cha nne cha mkutano wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China, CPC.

  Amesema mkutano huo ulitoa mpango wa ngazi ya juu wa wazi kuhusu mageuzi ya kina katika zama mpya, na kutaka juhudi za kufanya mageuzi zilenge kudumisha na kuboresha mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa Kichina, na kuufanya wa kisasa mfumo wa China na uwezo wa uongozi.

  Mkutano huo ulihudhuriwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang na viongozi wengine pamoja na wajumbe wote wa Kamati ya Mageuzi ya Kina.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako