• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa mataifa waona maendeleo kwenye utoaji wa dawa za tiba ya UKIMWI

  (GMT+08:00) 2019-11-27 08:45:40

  Ripoti iliyotolewa mjini Nairobi na tume ya kupambana na UKWIMI ya Umoja wa Mataifa UNAIDS inaonesha kuwa upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya HIV umepata maendeleo makubwa.

  Ripoti hiyo inaonesha kuwa hadi kufikia katikati ya mwaka huu watu milioni 24.5 kati ya milioni 37.9 wanaoishi na virusi vya Ukimwi duniani wanapata matibabu, na idadi ya watu wanaokufa kwa ugonjwa huo inazidi kupungua.

  Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Bibi Winnie Byanyima amesema kwenye sehemu nyingi duniani, maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kupunguza vifo vinavyotokana na UKIMWI na kupunguza unyanyapaa hasa kwenye nchi za mashariki na kusini mwa Afrika.

  Hata hivyo Bibi Byanyima amesema licha ya maendeleo hayo, kutendewa haki, kutokuwa na usawa, kukataliwa haki za kiraia, unyanyapaa na ubaguzi vinakwamisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako