• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto na vijana zaidi 300 wafa kwa Ukimwi kila siku

    (GMT+08:00) 2019-11-27 09:45:16

    Ripoti kuhusu watoto na Ukimwi iliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, inaonyesha kuwa watoto na vijana karibu 320 wanakufa kila siku kutokana na sababu zinazohusiana na ugonjwa wa Ukimwi.

    Chanzo kubwa cha vifo hivyo ni upatikanaji mdogo wa matibabu ya ARV na ukosefu wa juhudi za kuzuia maambukizi, na asilimia 54 tu ya watoto wenye umri chini ya miaka 14 waishio na VVU katika mwaka 2018 walipata dawa za ARV.

    Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha upatikanaji wa matibabu ya ARV kwa watoto waishio na VVU ni asilimia 91 katika Asia Kusini, ikifuatiwa na asilimia 73 katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, asilimia 61 katika Afrika Mashariki na Kusini, na asilimia 28 tu katika Afrika Magharibi na Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako