• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa ripoti kuhusu kazi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

  (GMT+08:00) 2019-11-27 18:16:23

  China leo imetoa ripoti ya mwaka 2019 kuhusu sera na hatua zake za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Naibu waziri wa mazingira ya China Bw. Zhao Yingmin amesema, tangu mwaka jana, China imepunguza utoaji wa hewa yenye Carbon kwa mfululizo, na itaendelea kudhibiti utoaji wa hewa zinazoweza kuongeza joto duniani, na kuhimiza maendeleo yasiyoleta uchafuzi.

  Tangu mwaka 2009, China imekuwa ikitoa ripoti kuhusu juhudi zake za kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabianchi kwa miaka 11 mfululizo. Ripoti ya mwaka huu imeeleza sera, hatua na kazi za China katika kukabiliana na suala hilo pamoja na mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka jana. Bw. Zhao anasema,

  "Kwa miaka mingi iliyopita, tumechukulia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama hatua muhimu ya kulinda mazingira ya kiikolojia, kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu ya uchumi, na kujenga China nzuri, na kutekeleza hatua mbalimbali madhubuti. Tangu mwaka jana, China imeendelea kusukuma mbele kazi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuchukua sera na hatua mbalimbali za kivitendo, ili kupunguza utoaji wa hewa zinazoweza kuongeza joto. China pia imesukuma mbele kazi ya kuzoea mabadiliko ya tabianchi, kukamilisha mfumo na utaratibu husika, kujenga biashara ya hewa yenye Carbon, na kuinua mwamko wa wananchi kuhusu suala hilo."

  Bw. Zhao amesema serikali ya China imeshiriki kwenye juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa hatua ya kiujenzi, kwa kufuata kanuni ya majukumu ya pamoja lakini yenye tofauti kutokana na ukubwa wa uwezo iliyowekwa na "Makubaliano ya Mwongozo ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi". Anasema,

  "Pia tumeendelea kuimarisha mazungumzo na ushirikiano na pande mbalimbali katika suala la mabadiliko ya tabianchi, kutoa misaada kadiri tuwezavyo kwa nchi zinazoendelea, kufanya ushirikiano wa kina kati ya nchi za kusini, kushikilia utaratibu wa pande nyingi, na kutia nguvu na uhai kwa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhifadhi mazingira ya kiikolojia."

  Bw. Zhao amesema ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea, China siku zote inashikilia kithabiti utaratibu wa pande nyingi, kutimiza ahadi zake zilizotolewa kwa kufuata hali yake maalumu, na kusukuma mbele mchakato wa mazungumzo ya pande nyingi kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa hatua za kiujenzi.

  Kuhusu mkutano wa 25 wa nchi zilizosaini Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika hivi karibuni, Bw. Zhao amesema China itaendelea kufanya kazi za kiujenzi, na kuunga mkono mkutano huo kupata matokeo mazuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako