• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatetea hatua zake za kupambana na ugaidi na kuondoa itikadi kali mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-11-27 19:37:13

    China imekosoa kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kuhusu Xinjiang, akisema kauli hiyo imejaa upendeleo wa kisiasa na haina ukweli, pia inaonyesha vigezo viwili alivyo navyo katika suala la kupambana na ugaidi na kuondoa itikadi kali.

    Habari zinasema, jana, Bw. Pompeo alisema kuna vitendo vya kukiuka vibaya haki za kibinadamu mkoani Xinjiang, akitoa wito kwa serikali ya China kuwaachia huru wote wanaoshikiliwa bila hatia.

    Bw. Geng amesema Xinjiang haina suala la kikabila, kidini wala haki za kibinadamu, na serikali ya mkoa huo inachukua hatua za kupambana na ugaidi na kuondoa msimamo mkali. Pia amesema serikali ya China inalinda uhuru wa kuabudu wa watu wa makabila mbalimbali madogo wakiwemo watu wa kabila la Xinjiang Uyghur, na inawakaribisha watu wa nje wenye msimamo wa kutopendelea upande wowote kutembelea na kujionea hali halisi mkoani Xinjiang.

    Bw. Geng amesisitiza kuwa mambo ya Xinjiang ni ya ndani ya China na hayapaswi kuingiliwa na pande zenye chuki dhidi ya China, na China itaendelea kujenga vizuri mkoa huo ili kuleta ustawi, utulivu, mshikamano wa kikabila na masikilizano ya kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako