• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la seneti Kenya launga mkono mpango wa Wizara ya fedha kuzinyima baadhi ya kaunti fedha

    (GMT+08:00) 2019-11-27 20:13:34

    Mpango wa Wizara ya Fedha ya Kenya wa kuzinyima fedha serikali 15 za kaunti ambazo hazijalipa madeni yao umepata uungwaji mkono Jumanne kutoka kwa maseneta.

    Wanachama wa Kamati ya Seneti kuhusu Fedha na Bajeti wamesema hatua hiyo itakuwa funzo kwa kaunti ambazo zimekuwa zikiwadhulumu wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuchelewesha malipo yao.

    Bunge hilo limesema mpango huo utakuwa afueni kwa wafanyabiashara wadogowadogo mashinani kwani wengi wao wakiwa vijana na akina mama. Aidha kamati hiyo imesema tayari wamepokea stakabadhi kutoka kwa waziri wa fedha na ombi la kutaka wizara ichukua hatua dhidi ya kaunti zilizokataa kulipa madeni tangu 2013. Kulingana na Bw Yatani, kufikia mwaka huu wa kifedha wa 2019/2020 wakandarasi na wafanyabiashara mbalimbali walikuwa wakizidai kaunti hizo jumla ya Sh51 bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako