• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafafanua mpango wake kuhusu suala la Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2019-11-27 20:14:30

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na wageni waliohudhuria Baraza la Usalama kuhusu usalama wa Mashariki ya Kati.

    Bw. Wang amesema, mpango wa China kuhusu usalama wa Mashariki ya Kati ni kujenga mfumo endelevu wa pamoja, jumla na kushirikiana wa usalama, badala ya mawazo ya kujipatia tu usalama, kujaribu kupata usalama kabisa, kushindana na kujigamba

    Pia amesema, inapaswa kushikilia njia sahihi ya utatuzi wa kisiasa, kulinda kanuni ya usawa na haki, kusimamia kanumi ambazo kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na kufanya juhudi kwa pamoja kwa sehemu mbalimbali na jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Wang amesema, China haiingilii kati mambo ya ndani ya nchi za Mashariki ya Kati, na itaendelea kufanya juhudi kusaidia kujenga amani, kuhimiza utulivu, na kutoa mchango kwa maendeleo ya Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako