• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vanila kuleta mabadiliko kiuchumi

    (GMT+08:00) 2019-11-27 20:18:34

    Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania unasemekana kupata mabadiliko ya kiuchumi kwa kusajili Umoja wa Wakulima wa Vanila chini ya kanuni namba 14(2) kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya Mwaka 2013.

    Hayo yalibainishwa kwenye kikao cha ushauri cha mkoa wa Kilimanjaro, chini ya uongozi wa Dk. Anna Mghwira.

    Bi Anna amesema uwekezaji huo utaleta mabadiliko ya kiuchumi ikiwemo kukuza uchumi wa nchi.

    Alisema lengo la kusajili umoja huo ni kuwaimiza wakulima kujikita katika kulimo cha Vanilla, kwani hutumika kwenye kutengeneza harufu mbalimbali pamoja na kwenye viwanda vya kutengeneza dawa za matibabu ya binadamu.

    Hivi sasa bei ya Vanila ni kuanzia Sh. 4,000 hadi 30,000/- kwa vanila mbichi na kutoka Sh. 300,000 hadi Sh. 800,000 kwa kilo moja ya vanilla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako