• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kilimo cha pamba Kenya kuanza kupata mafanikio

    (GMT+08:00) 2019-11-27 20:20:24

    Kilimo cha Pamba nchini Kenya huenda kikawapa wakulima wa zao hilo wafaida zaidi. Hii ni baada ya ujumbe wa kampuni ya Thika Cloth Mills, kuzuru eneo la Nyanza kwa ajili ya kutafuta bidhaa hiyo kwa kununua kutoka kwa wakulima.

    Ujumbe wa watu wanane kutoka kampuni hiyo ulizuru kaunti za Homa Bay, Kisumu na Siaya kwa lengo la kutafuta soko la kununua pamba kwa wingi.

    Hivi sasa kampuni mbili za kuunda nguo za majora; Thika Cloth Mills na SunFlag Textile pamoja na Knit Wear Manufacturing Ltd zimejitolea kununua pamba kutoka kaunti kadha za eneo la Nyanza.

    Mkurugenzi wa Thika Cloth Mills Bi Tejal Dhodhia alithibitisha kuwa serikali imejitolea kuona ya kwamba wakulima wanapewa mbegu za pamba na dawa za kupuliza kwa zao hilo la pamba. Kampuni hiyo ya kushona majora ya nguo imepewa zabuni na serikali kushona nguo za idara ya usalama. Meneja mkuu wa kampuni ya SunFlag Textile na Knitwear Manufacturing Ltd, Bw Vassan Shah, alisema kampuni hiyo imekuwa ikinunua pamba kwa wingi kutoka Uganda lakini watalenga kuzuru maeneo tofauti kukutana na wakulima wa pamba hapa nchini ili wanunue bidhaa hiyo kutoka kwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako