• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNDP yapongeza kasi ya ukuaji wa uchumi Zanzibar

  (GMT+08:00) 2019-11-27 20:22:01

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) limepongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Zanzibar.

  Mwakilishi UNDP Zanzibar, Christine Musisi, alieleza kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Mohamed Shein shirika hilo limeona mageuzi makubwa ya kiuchumi, kimaendeleo na kuimarika kwa utawala bora.

  Alisema kuwa UNDP litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza na kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili Zanzibar izidi kupata mafanikio.

  Aidha, mwakilishi huyo alieleza kuwa katika uongozi wa Rais Shein, Zanzibar imeweza kushuhudia mafanikio makubwa ya kimaendeleo ikiwamo juhudi za kupambana na umaskini na kukuza uchumi. Naye Rais Shein alieleza kuwa uchumi wa Zanzibar umezidi kuimarika kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wake bila ya kuwasahau washirika wa maendeleo ikiwamo UNDP.

  Aidha, alieleza juhudi na mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha na kukuza uchumi wake ikiwa ni pamoja na kuiimarisha sekta ya uwekezaji, viwanda sambamba na kuiendeleza na kuiimarisha sekta ya utalii ambayo inachangia kwa asilimia 27 ya Pato la Taifa la Zanzibar na asilimia 80 ya fedha za kigeni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako