• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe akagua ujenzi wa jengo jipya la bunge

  (GMT+08:00) 2019-11-28 09:22:01

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametembelea eneo la ujenzi wa jengo jipya la bunge linalojengwa kwa msaada wa China, na kuishukuru China kwa msaada inaotoa kwa Zimbabwe katika muda mrefu uliopita.

  Rais Mnangagwa amesema katika miaka ya hivi karibuni, China imeisaidia Zimbabwe kujenga jengo jipya la bunge, hospitali ya Mahusekwa na miradi mingine mingi ambayo imesaidia Zimbabwe kuboresha miundo mbinu na hali ya ukosefu wa nishati. Amewataka wahandisi na wafanyakazi wa Zimbabwe kujifunza kutoka kwa wafanyakazi wa China, ili kuinua kiwango chao.

  Habari nyingine zinasema makamu wa rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga pia ametembelea eneo hilo akiambatana na rais Mnangagwa. Hii ni mara ya kwanza kwake kuonekana hadharani baada ya kurudi kazini akitokea kwenye matibabu ya miezi minne nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako