Mabingwa watetezi Liverpool watahitaji angalau pointi moja kwenye mchezo wao wa mwisho wa kundi F ili kuihakikishia kuingia hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa baada ya kutoka sare dhidi ya Napoli. The Red wangekuwa vinara wa kundi lao F kama wangeshinda lakini waliachwa nyuma katika kipindi cha kwanza baada ya Dries Mertens kutingisha wavu dakika ya 21 na kuwafanya Liverpool kutaharuki katika kipindi chote cha kwanza. Liverpool ambao hawakuonesha soka safi sana katika kipindi cha kwanza walitapa sana na kujitahidi kulipiza kisasi kwa kusawazisha baada ya kurejea tena katika kipindi cha pili, goli ambalo lilitundikwa na Dejan Lovren. Hata hivyo sare hiyo haikuishia kwenye mechi hiyo tu, kwani hata kwa upande wa Chelsea dhidi ya Valencia pia hakuna aliyeweza kumtambia mwenziwe. Mchezo wao ulimalizika kwa sare ya 2-2.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |