• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe akagua mradi wa jengo la bunge linalojengwa na kampuni ya China

  (GMT+08:00) 2019-11-28 17:00:08

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amekagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya la bunge la nchi hiyo linalojengwa na kampuni ya China na kusifu kasi ya ujenzi huo na manufaa yatakayoletwa kwa watu wa Zimbabwe.

  "Mradi huu ni muhimu kwa Zimbabwe. China inatusaidia kujenga jengo la kisasa la bunge. Tunaishukuru sana China. Tunajua kwamba, katika mchakato wa maendeleo ya uchumi na viwanda vya kisasa vya Zimbabwe, tunawajibika kutafuta watu wanaopenda kusaidia na kuunga mkono maendeleo ya nchi yetu."

  Katika hotuba yake, rais Mnangagwa ametaja miradi mingi ya ushirikiano wa China na Zimbabwe, akisema:

  "China imeshirikiana na sekta mbalimbali za Zimbabwe. Licha ya mradi huu wa jengo la bunge, China pia imefanya miradi ya ukarabati wa uwanja wa ndege wa Vicotria Falls, upanuzi wa kituo cha uzalishaji umeme kwa nguvu ya maji cha Kariba, na upanuzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya moto cha Hwange No. 7 na 8. China pia imetoa mkopo kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare. Serikali, chama tawala na watu wa Zimbabwe wote wanashukuru uhusiano mzuri na China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako