• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Ajira za muda 14,900 zapatikatana wakati wa maonesho ya kimataifa

  (GMT+08:00) 2019-11-28 19:20:22

  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TanTrade), imebainisha kwamba ajira za muda mfupi 14,912 zilipatikana kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) mwaka huu.

  Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Mohammed Hamis wakati akieleza mafanikio ya mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano.

  Amezitaja ajira zilizopatikana kuwa ni pamoja na ujenzi, ulinzi na usafi huku mauzo ya papo kwa hapo kwenye maonyesho hayo yakiwa ni zaidi ya Sh209.4 milioni.

  Amesema Kampuni 437 zilipata oda ya kufanya biashara (Business deals) zenye thamani ya Sh7.93 bilioni.

  Amesema maonyesho hayo yalivutia watembeleaji 260,037 kutoka ndani na nje ya nchi huku upatikanaji wa mapato ya Serikali kutokana na kodi mbalimbali ikiwemo VAT, ushuru wa forodha na kodi ya uingizaji bidhaa zikiongezeka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako