• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EPZA yatoa wito wa kuwa na programu ya kuandaa wafanyakazi kwa kazi za viwandani

    (GMT+08:00) 2019-11-28 19:28:54

    Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) imesema Tanzania inaweza kuwa eneo bora zaidi la uwekezaji na kuvutia wawekezaji wengi endapo itakuwa na programu maalum ya kuandaa wafanyakazi wenye ujuzi wa kazi za viwandani.

    Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alisema Tanzania na nchi na nyingine za Afrika zina kila kitu kinachotakiwa na wawekezaji zikiwamo malighafi, vyanzo vya kutosha vya umeme, ardhi ya kutosha na soko kubwa, lakini kukosekana kwa wafanyakazi wenye ujuzi unaotakiwa katika viwanda imekuwa kikwazo kikubwa cha kuvutia uwekezaji zaidi.

    Simbakalia alisema hayo wakati akiongea na wahadhiri waandamizi kutoka vyuo 16 vya ufundi vya nchi tatu za Afrika, Tanzania, Kenya na Ethiopia ambazo zinashiriki katika mradi wa Eastern Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

    Aliwataka wahadhiri waandamizi na vyuo vyao kuelekeza nguvu zaidi kuwaandaa vijana watakaokuwa na ujuzi wa kazi za viwandani ikiwa ni hitaji kubwa kwa wawekezaji wa viwanda kutoka sehemu mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako