• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Vijiji 8,000 vyafikiwa na umeme Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-11-28 19:32:07

    Wakala wa Umeme Vijijini (REA), umetumia Sh. trilioni 2.3 kusambaza umeme katika vijiji 8,000 kati ya 12,268 nchini.

    Aidha, wakala huo kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) itafanya tathmini ya watumiaji wa nishati hiyo kwenye maeneo ya vijijini.

    Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Amos Maganga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari..

    Alisema kabla ya REA kuanza mwaka 2017 asilimia mbili ya vijiji ambayo ni sawa na vijiji 518 vilikuwa na umeme.

    Kuhusu tathmini hiyo, Maganga alisema lengo la tathmini hiyo ni kujua kama umeme unatumika ipasavyo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

    Alisema tathmini hiyo itajumuisha watu kutoka Wizara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kila mmoja atasimama kwa nafasi yake na pia wataangalia wapi panahitaji kuboresha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako