• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga vikali Marekani kusaini mswada kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-11-28 19:49:33

    Wizara ya mambo ya nje wa China leo imetoa taarifa ikipinga vikali Marekani kusaini mswada wa haki ya binadamu na demokrasia ya Hong Kong na kuuidhinisha kuwa sheria.

    Wizara hiyo imesema, kitendo hicho kinaingilia kati mambo ya Hong Kong, ambayo pia ni mambo ya ndani ya China, kinakiuka sheria ya kimataifa na kanuni ya msingi ya uhusiano wa kimataifa, na serikali na watu wa China wanapinga thabiti kitendo hicho cha kimabavu.

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Le Yucheng amemwita balozi wa Marekani nchini China Bw. Terry Branstad, na kutoa malalamiko makali kwa hatua ya Marekani kusaini mswada huo.

    Habari nyingine zinasema, serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong leo imepinga vikali kusainiwa kwa mswada wa haki ya binadamu na demokrasia ya Hong Kong na mswada mengine kuhusu Hong Kong na kuiidhinisha kuwa sheria, ambazo zinatoa uelewa mbaya kwa waandamanaji, na pia hazisaidii kutuliza hali ya Hong Kong, badala yake, zitaathiri vibaya uhusiano kati ya pande hizo mbili na maslahi ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako