• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Mwakinyo, Tinampay hapatoshi leo Uhuru

  (GMT+08:00) 2019-11-29 18:12:16

  Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu nchini Tanzania imewadia, ambapo usiku huu bondia Hassan Mwakinyo atapambana na Mfilipino Arnel Tinampay katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Pambano hilo la uzito wa Super Welter lisilo na ubingwa ni la raundi 10, na ni la kwanza la kimataifa kwa Mwakinyo kucheza katika ardhi ya Tanzania. Pambano lake la mwisho lilikuwa Machi mwaka huu nchini Kenya, ambapo alimshinda kwa Technical Knock Out mpinzani wake Sergio Gonzalez kutoka Argentina. Akizungumzia pambano lake la leo, Mwakinyo amesema licha ya kukutana na bondia anayetokea kwenye gym ya bondia mkubwa duniani, Manny Pacquiao, lakini haoni cha kumtisha na kumnyima ushindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako