• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa serikali ya Xinjian avilaumu vyombo vya habari vya kigeni kwa kuandika habari zisizo sahihi kuhusu mkoa huo

    (GMT+08:00) 2019-11-29 18:55:58

    Msemaji wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur amesema, kitendo cha vyombo vya habari na mashirika ya kigeni kuandika habari za uwongo juu ya waraka unaodaiwa kuvujishwa kuhusu Xinjian kinakiuka ukweli, na hakikubaliki.

    Amesema vituo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi mkoani humo vimeanzishwa kwa kufuata sheria, na sio makambi maalum, na kuongeza kuwa wanafunzi hawana vizuizi vyovyote na uhuru wao haujazuiliwa, na haki za wanafunzi katika vituo hivyo inalindwa kikamilifu kuendana na sheria. Amesema imekubalika kuwa vituo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi mkoani Xinjian vinaendana na mahitaji na kanuni za Umoja wa Mataifa katika kuzuia na kupambana na ugaidi, na kulinda haki za kimsingi za binadamu, na zinastahili kutambuliwa rasmi.

    Amesema hakuna kesi zozote za vurugu na ugaidi zilizotokea mkoani Xinjian kwa miaka mitatu iliyopita, ikiwa ni ishara nzuri ya maendeleo ya uchumi, utulivu wa jamii, umoja wa kitaifa na uhuru wa kuabudu katika mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako