• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania na Rwanda zakaribia mwisho wa mazungumzo kuhusu SGR

  (GMT+08:00) 2019-11-29 19:00:55

  Serikali za Tanzania na Rwanda ziko katika mazungumzo ya mwisho ya ujenzi wa reli ya wastani (SGR) kutoka bandari kavu ya Isaka nchini Tanzania hadi Rwanda.

  Rais wa Tanzania John Magufuli amesema reli hiyo pia itahudumia nchi ambazo hazipakani na bahari kama vile Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

  Alisema uchunguzi yakinifu wa SGR inayounganisha Tanzania na Rwanda tayari umefanywa, na kuongeza kuwa nchi hizo mbili zinatafuta wafadhili wa mradi huo.

  Jumatatu, Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB) ambayo ni taasisi ya biashara na maendeleo barani Afrika, ilidhinisha mkopo wa dola bilioni moja kwa Tanzania kwa utekelezaji wa miradi ya miundombinu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako