• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wakulima kusajiliwa ili kutambua kazi zao

  (GMT+08:00) 2019-11-29 19:01:19

  Serikali ya Tanzania imeandaa utaratibu wa kuwasajili wakulima wote nchini na kutambua kilimo wanachokifanya.

  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, aliyasema hayo wakati wa kongamono la kilimohai, kwa kuwa utaratibu huo utasaidia kujua idadi yao nchini.

  Alisema serikali inatambua jitihada za wakulima hasa wale wanaolima kilimohai, ambacho mazao yake yanahitajika zaidi kwa ajili ya kuokoa afya za watu.

  Waziri huyo alisema kama watu watalima kilimohai kwa njia ya asili wataepusha jamii na magonjwa na kuipunguzia mzigo serikali.

  Alisema serikali itakuwa karibu na wakulima wa kilimohai kuhakikisha kilimo hicho kinaendelezwa kwa manufaa ya wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako