• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: EAC yatakiwa kuimarisha umoja na mazingira ya biashara

    (GMT+08:00) 2019-11-29 19:04:09

    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi, amezishauri nchini wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuimarisha umoja kwa maslahi ya watu wake.

    Vilevile, amewashauri wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo kufanya biashara kwa maslahi ya uchumi wa wananchi wa jumuiya hiyo.

    Prof. Kabudi alitoa ushauri huo jana jijini Arusha alipofungua Mkutano Mkuu wa Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki na Wawekezaji katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

    Alizitolea mfano nchi za Ujerumani, Sweden, Denmark na Norway ambazo alidai wawekezaji na wafanyabishara wa sekta binafsi wamejikita katika uchumi wa kijamii ili kusaidia kukuza uchumi wa mataifa hayo.

    Aliwataka wawekezaji hao kuachana na taratibu za nyuma na kuanza kuchukua hatua za kushirikiana kujikita kwenye biashara za kukuza uchumi wa kijamii zaidi ili kufikia lengo la kukuza uchumi wa mataifa hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako