• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kuadhimisha miaka 10 ya ushirikiano kati ya China na FAO wafanyika nchini Uganda

  (GMT+08:00) 2019-11-29 19:21:04

  Mkutano wa ngazi ya juu wa kuadhimisha miaka 10 ya ushirikiano wa nchi za kusini kati ya China na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO umefanyika mwanzoni mwa wiki hii mjini Kampala, Uganda, ambapo makubaliano ya pande tatu kati ya China, Uganda na FAO yalisainiwa.

  Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, rais Yoweri Museveni wa Uganda ameishukuru China kwa kutoa misaada isiyo na masharti na mchango katika kupunguza umaskini nchini Uganda. Pia ametoa ushauri wa jinsi ya jukwa la ushirikiano wa nchi za kusini na linavyoweza kuhimiza ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Uganda.

  Naye mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu amepongeza mchango uliotolewa na China katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Amezitaka nchi zilizoendelea kushirikiana na nchi zinazokabiliwa zaidi na njaa kuzisaidia kupata maendeleo. Pia ameeleza matarajio yake kuwa, pande mbalimbali kuendelea kuongeza ushirikiano na kupanua wenzi wa kimkakati kwa njia shirikishi

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako