Fabio Cannavaro amejibebea heshima kubwa kama kocha kwa kubeba taji la kwanza kwenye Ligi Kuu ya China akiwa na klabu ya Guangzhou Evergrande wiki kadhaa baada ya kudhaniwa kuwa atatimuliwa kazini. Cannavaro anayeifunza Guangzhou Evergrande iliyochukua taji lake la nane alikaa pembeni kwa muda mwishoni mwa Oktoba na kuhudhuria "darasa la ushirikiano wa utamaduni". Mmiliki wa klabu baadaye akaamua kumrejesha kama meneja baada ya kukubali kujitathmini upya. Guangzhou Evergrande jana walivaana na Shenhua ambayo ni ya pili kutoka mwisho katika msimamo wa ligi na kuishinda 3-0. Beijing Guoan walikuwa nyuma kwa pointi mbili na kuchukua nafasi ya pili huku upande wa Rafael Benitez Dalian Yifan wakimaliza wa tisa. Cannavaro, aliyekuwa nahodha wa Italia na kubeba kombe la dunia mwaka 2006, amekuwa akishutumiwa na klabu yake kwa kuwa na uwezo mdogo wa kurekebisha makosa na kuwashughulikia vibaya wachezaji wake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |