• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Norwich na Arsenal watamatisha mechi kwa sare ya 2-2

  (GMT+08:00) 2019-12-02 08:27:39

  Mechi kati ya Norwich na Arsenal ilitamatika kwa sare ya 2-2 huku Gunners wakiandikisha matokeo mabovu kwenye Ligi Kuu tangu mwaka 1975. Pierre-Emerick Aubameyang aliifungia Arsenal mabao mawili baada ya Teamu Pukki na Todd Cantwell kuiweka Canneries kifua mbele kwa mabao mawili. Pukki ndiye alifunga bao la kwanza kwenye dakika ya 21. Dakika mbili baadaye Arsenal walitunikiwa mkwaju wa penalti baada ya Christoph Zimmerman kushika mpira. Kipindi cha kwanza kikielekea kutamatika, Cantwell alisawazisha magoli yao kuwa 2-1. Aubameyang alisawazisha bao hilo katika kipindi cha pili baada ya kutumia vizuri kona ambayo haikuwa imepanguliwa vyema na kubadilisha matokeo kuwa 2-2. Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Freddie Ljungberg tangu kumrithi Unai Emery kama kocha wa muda wa Gunners.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako