Mwanariadha kutoka Uganda Joshua Cheptegei amevunja rikodi ya dunia katika mbio za km 10 huko Valencia, na kuandikisha muda mpya wa dakika 26 na sekunde 38. Mwanariadha huyo mwenye miaka 23 amevunja rikodi ya zamani kwa sekunde sita, ambayo iliwekwa mwaka 2010 na Mkenya Leonard Komon. Cheptegei amevikwa taji la bingwa wa mita 10,000 huko Doha mwezi Oktoba, na pia mwezi Machi kushinda taji la dunia la mbio za nyika km 10 nchini Denmark. Mwaka 2018 alikimbia kwa dakika 41 sekunde tano huko Nijmegen, Uholanzi, na kuvunja rikodi ya dunia ya mbio za km 15. Kasi ya wastani ya Cheptegei ilikuwa ni dakika mbili na sekunde 40 kwa kilomita huko Valencia, na kukamilisha kilomita 5 kwa kutumia dakika 13 na sekunde 24.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |