• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya abiria ya Cameroon yashambuliwa wakati ikitua kwenye eneo la watu wanaotumia Kiingereza

    (GMT+08:00) 2019-12-02 08:32:46

    Ndege moja ya abiria ya Cameroon jana ilishambuliwa kwenye Uwanja wa ndege wa Aamenda, ulioko kwenye eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo wanakoishi watu wanaotumia lugha ya Kiingereza. Watu wenye silaha waliifyatulia risasi ndege hiyo ya Shirika la ndege la nchi hiyo Camair iliyokuwa inatua uwanjani.

    Hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye shambulizi hilo, lakini risasi zilipiga bawa la kushoto na kutoboa kabati la ndege hiyo. Ofisa mmoja alisema vikosi vya usalama vilijibu haraka na kuzuia shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako