• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China azungumza na mwenyekiti wa Tume ya Ulaya

  (GMT+08:00) 2019-12-02 09:38:39

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenyekiti wa Tume ya Ulaya Bibi Ursula von der Leyen, na kujadili uhusiano na ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo utaratibu wa pande nyingi, biashara huria na mabadiliko ya tabianchi. Bw. Li amempongeza Bibi von der Leyen kwa kuwa mwenyekiti, na kusema kuongeza uratibu wa kimkakati na ushirikiano katika sekta zote kati ya China na Umoja wa Ulaya kutanufaisha pande hizo mbili na hata dunia nzima. Bibi von der Leyen amesema Umoja wa Ulaya unazingatia uhusiano kati yake na China, na kuna maslahi mengi ya pamoja katika masuala mbalimbali ikiwemo maendeleo endelevu na mazungumzo kuhusu uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako