• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Palestina yailaani Marekani kwa kuunga mkono Israel kujenga makazi mapya

  (GMT+08:00) 2019-12-02 09:39:28

  Palestina imelaani Israel kwa uamuzi wake wa kujenga makazi mapya mjini Hebron kusini mwa Kando ya Magharibi ya Mto Jordan. Katibu mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina Bw. Saeb Erekat amesema, uamuzi huo ni matokeo halisi ya kwanza kwa Marekani kuhalalisha ukoloni, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua ikiwemo vikwazo dhidi ya uamuzi huo. Ujenzi wa makazi ya wayahudi kwenye sehemu za Palestina unachukuliwa na nchi nyingi na sheria za kimataifa kama ni kitendo haramu, na hii pia ndio sababu kuu ya kusababisha kushindwa kwa mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel mwaka 2014.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako