• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China aongea na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2019-12-02 17:21:41

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana ameongea kwa njia ya simu na mwenyekiti mpya wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leye.

    Kwenye mazungumzo yao, Bw Li amesema China na Ulaya ni wenzi muhimu wa ushirikiano, na pande zote mbili zinalinda kithabiti utaratibu wa pande nyingi na biashara huria. Amesema China siku zote inaunga mkono kithabiti mchakato wa kuhimiza umoja wa nchi za Ulaya, itatekeleza kithabiti Makubaliano ya Paris, na kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na nchi za Ulaya katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Naye Bibi Ursula von der Leye amesema mazungumzo hayo yanaonyesha kuwa Ulaya inatilia maanani uhusiano na China. Amesema anatarajia kuhudhuria mkutano wa 22 wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na China utakaofanyika nchini China mwakani. Ameongeza kuwa, Kamati ya awamu mpya ya Umoja wa Ulaya inapenda kushirikiana na China juu ya masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako