• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekebisho ya Kanuni ya utekelezaji wa sheria kuhusu usalama wa chakula ya China yatekelezwa rasmi

    (GMT+08:00) 2019-12-02 18:04:37

    Marekebisho ya kanuni ya utekelezaji wa sheria ya usalama wa chakula nchini China yameanza kutekelezwa rasmi mwezi huu. Kanuni hii imeimarisha adhabu kwa ukiukaji wa sheria na kanuni kuhusu usalama wa chakula…

    Ikiwa kanuni inayolingana na sheria ya usalama wa chakula, marekebisho ya kanuni hiyo yanaweka mkazo katika kufafanua kanuni halisi kuhusu sheria ya usalama wa chakula, kuimarisha adhabu kwa ukiukaji wa sheria na kanuni, kutangaza hatua za usimamizi kuhusu masuala halisi, kuboresha mfumo wa usimamizi wa hatari, na kuimarisha vitendo vya usimamizi kwa ufanisi. Naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya usimamizi wa soko la China Bibi Sun Meijun anasema:

    "Awali, viwanda viliadhibiwa kwa suala la ukosefu wa usalama wa chakula, hatua ambayo haina ufanisi. Kwa mujibu wa marekebisho mapya, kwa vitendo vya kukiuka sheria kwa makusudi na kuleta athari mbaya, si kama tu makampuni yataadhibiwa, wakuu wa makampuni pamoja na wahusika wengine muhimu pia wataadhibiwa, na kiwango cha juu cha faini kitafikia mara kumi ya mapato yao waliyoyapata mwaka uliopita kutoka kampuni yao."

    Mbali na hayo, kanuni hiyo pia inatoa adhabu ya kijinai kwa makampuni yanayokiuka sheria kwa makusudi na kuleta athari mbaya, kuongeza fidia kwa wateja, na kutoa bonasi kwa watu wanaoripoti hali ya ukiukaji wa sheria ndani ya makampuni, na kuanzisha utaratibu wa pamoja wa kuhamasisha vitendo vya kuimarisha uaminifu na kutoa adhabu kwa ukosefu wa uaminifu. Pia kulinganisha hali ya uaminifu wa usalama wa chakula na kanuni za kuingia kwenye masoko, kukusanya fedha na kutoa mikopo, na kuzitangaza hali zinazohusika hadharani. Naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya usimamizi wa soko la China Bibi Sun Meijun anasema:

    "Muamana ni msingi kwa makampuni kushindana kwenye soko. Lengo la kanuni hiyo ya kuanzisha mfumo wa pamoja wa kuhamasisha uaminifu na kuadhibu ukosefu wa uaminifu, na utaratibu wa kuorodhesha wazalishaji wanaokiuka vibaya sheria ni kuwaondoa wale wanaokosa uaminifu."

    Wataalamu wameeleza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni hali ya usalama wa chakula nchini China imeboreshwa siku hadi siku, lakini sekta hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Marekebisho ya kanuni yatachangia katika kuinua kwa ufanisi kiwango cha jumla cha usalama wa chakula nchini China kwa pamoja na Sheria ya usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako