• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la mtiririko wa Mto Changjiang kuwa uwanda mpya wa juu wa China kufungua mlango kwa nje

    (GMT+08:00) 2019-12-02 18:56:34

    Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali la China hivi karibuni zimetoa waraka wa mwongozo wa mipango ya maendeleo ya mafungamano ya eneo la mtiririko wa Mto Changjiang, unaohusu maendeleo ya eneo hilo katika miaka 5 hadi 15 ijayo.

    Waraka huo umefafanua upande mpya na hatua mpya za eneo hilo katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na nchi za nje, na kutoa ishara muhimu ya China kupiga hatua thabiti katika kufungua mlango kwa pande zote.

    Kwa mujibu wa waraka huo, eneo la mtiririko wa Mto Changjiang litakuwa sehemu muhimu ya majaribio kwa China kufanya raundi mpya ya kufungua mlango kwa nje. Pia litahimiza ushirikiano na uwekezaji wa China nje ya nchi kupanda ngazi ya juu zaidi, na kuwa mfano mzuri katika kujenga mazingira mazuri ya kufanya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako