• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na katibu wa baraza la usalama la Russia

  (GMT+08:00) 2019-12-02 19:21:00

  Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na katibu wa baraza la usalama la Russia Bw. Nikolai Patrushev mjini Beijing.

  Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amesema, tangu mwaka huu, nchi za magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani zimeingilia zaidi mambo ya ndani ya China na Russia, kitendo ambacho kimezuia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hizo mbili. Anaamini kuwa hakuna nguvu inayoweza kuzuia maendeleo ya watu wa nchi hizo, na pia hawataathiriwa na nguvu za nje. Amesema China na Russia zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya usalama na kuhimiza uaminifu wa kimkakati.

  Naye Bw. Patrushev amesema, pande hizo mbili zinatakiwa kuimarisha kazi ya uratibu, kulinda mamlaka na usalama wa nchi, kulinda utulivu wa mkakati wa kimataifa, kuhimiza mwelekeo wa pande nyingi duniani na demokrasia ya uhusiano wa kimataifa, na kulinda sheria za kimataifa na utaratibu wa kimataifa wenye haki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako