• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Suleiman Matola kurudi Msimbazi, Polisi Tanzania wasubiri kulipwa fidia

  (GMT+08:00) 2019-12-02 20:40:09

  Mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba (Simba SC), wapo katika mpango wa kutaka kumng'oa kocha wa Polisi Tanzania FC Suleiman Matola, ili wamkabidhi jukumu la kuwa kocha mkuu. Uongozi wa Simba SC upo katika mpango huo, baada ya kuthibitisha kuachana na kocha Patrick Aussems. Matola anapewa kipaumbele cha kurithi mikoba ya kocha mkuu huko Msimbazi, kufuatia kuwa na uzoefu wa kutosha katika ligi ya Tanzania bara, pamoja na kuifahamu vyema klabu ya Simba, ambayo aliwahi kuitumikia kama mchezaji. Hata hivyo makamu mwenyekiti wa Polisi Tanzania FC Robert Munis, alipoulizwa kuhusu mpango huo wa mabingwa mara 20 wa Tanzania bara, alisema hakuna shaka yoyote endapo watakubaliana na uongozi wa Simba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako