• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa tumbaku Tanzania wazalishaji tumbaku nyingi zaidi ya malengo

    (GMT+08:00) 2019-12-02 20:53:35

    Wakulima wa tumbaku nchini Tanzania wamezalisha tumbaku kilo 69,757,425 katika msimu uliopita,hivyo kuwa zaidi ya lengo la uzalishaji kwa mujibu wa mkataba ambao ilikuwa kilo 57,305,127.

    Kutokana na hatua hiyo,serikali imepata kazi ya ziada ya kuhakikisha inawasaidia wakulima hao kupata soko la kilo 12,452,298 zilizozalishwa nje ya mkataba.

    Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Kilimo ,Japhet Hasunga,alipozungumza na waandishi wa habari.

    Alisema tumbaku iliyonunuliwa mpaka mwisho wa msimu huo wa mwaka 2018/2019 ndani ya mikataba ni kilo 60,691,972.21 zenye thamani ya dola za Marekani 92,927,331.79 sawa na asilimia 105.9 ya lengo.

    Aidha alisema jitihada za Wizara ya Kilimo kushirikiana na odi ya Tumbaku zilifanikiwa kushawishi kampuni ya Alliance One na Premium Active kununua tumbaku kilo 6,305,000 ,kuongeza kilo toka 4,200,000 hadi 7,400,000 mpaka sasa,ununuzi wa tumbaku hiyo iliyozidi malengo ya uzalishaji umefikia kilo 8,107,221 zenye thamani ya dola 6,330,174.

    Alisema tumbaku iliyobaki kwa wakulima bila mnunuzi ni kilo 3345,077 katika mkoa wa Tabora na kiasi kidogo Ushetu Shinyanga,ununuzi umekamilika kwa asilimia 100 mkoa wa Mbeya ,Songwe,Kigoma,Singida,Iringa,Ruvuma na Katavi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako